Loading...

5/15/2019

Dogo Janja afichua siri yake na Nandy


Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ amefichua siri yake na msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ kwa kusema kuwa akiwa naye popote pale familia yake huwa na amani.

Dogo Janja alisema kuwa, alijuana na Nandy kabla hata hajaanza muziki.

“Nandy ni mshikaji wangu tangu zamani sana. Nakumbuka tangu hajaanza muziki wala kushiriki yale mashindano ya kuimba ambayo yalimtoa (Tekno Own Stage) yaliowahi kufanyika nchini Kenya na Nigeria.

“Ujue damu zetu zinaendana sana na ni mtu ambaye hata familia zetu zinafahamiana. Leo Nandy atakuja kwetu na mimi hivyo hivyo kwao kwahiyo hata nikiwa naye popote familia yake inakuwa na amani kabisa,” alisema Dogo Janja.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger