Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amefanya ziara ya ghafla ya ukaguzi katika Hospitali Kuu ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam na kujionea namna hospitali hiyo inavyotoa huduma za matibabu kwa wananchi wanaofika hospitalini hapo.
Akizungumza na uongozi wa hospitali hiyo IGP Sirro amewataka waganga na wauguzi kufanyakazi za kitabibu kulingana na viapo vyao huku wakihakikisha wanatoa huduma bora za matibabu kwa wateja.
Aidha, IGP Sirro amekagua jengo la kuhifadhia maiti ambalo tayari limekamilika kwa kutoa huduma za kuhifadhi miili ya marehemu.
Wakati huo huo IGP Sirro amefanya ukaguzi wa ghafla na kukagua ujenzi wa majengo ya ghorofa unaotokanana fedha iliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alitoa kiasi cha fedha Tsh. Milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa Chuo cha Maofisa wa Polisi kilichopo kurasini jijini Dar es es Salaam.
