Misingi 4 ya kuifahamu kabla hujaanza Biashara



Mara nyingi baadhi yetu huwa tunaanza biashara kwa kusikia kwa watu faida ya biashara hiyo, bila hata kujua misingi halisi ya kabla kuanzia biashara husika tumejikuta Tukianza biashara hiyo na mwisho wa siku biashara hizo zimekuwa zikifa.

Lakini katika makala yetu hii ya leo tutaangalia misingi muhimu ya kuielewa mapema kabla ya kuanza biashara yoyote. Ili pindi tutakapoanza biashara hiyo tuweze kupata faida kwani tunakuwa umeelewa misingi yake.

Mambo hayo ya msingi tutakayojifunza hapa ni maalumu kwa ajili ya wote wanaotaka kuwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo pia. Kwa yeyote anahitaji kupata faida kubwa na kuepuka kupata hasara zisizo za lazima katika biashara yake, misingi hii ni muhimu sana kwake kuijua.

1. Eneo la kufanyia biashara.
Kwa kuwa ndio kwanza unaanza kufanya biashara lazima ufanye uchunguzi wa kutosha juu ya kile unatochotaka kukifanya. Eneo hili lakufanyia biashara  ni lazima ulichunguze kwa kuangalia uhitaji wa  wa wateja wa eneo husika.

Kwa mfano kama unataka kufanya biashara ya kuuza vifaa vya shule (stationery) lazima ujiulize ni wapi ambako unahisi ukiweka biashara yako kuna wateja wengi. Baada ya kufikiri unaweza ukaangalia kwenye maeneo ya shule,vyuo , kanisani na maeneo mengine.

Lakini hiyo haitoshi nenda sehemu husika jaribu kufanya uchunguzi ni vitu gani wanavifanya
wafanyabiashara wengine ambao wana biashara kama yako? Angalia ni changamoto gani wanazozipata ili pindi ukianza kufanya biashara hiyo ujue mbinu za kupambana na changamoto hizo kirahisi.

2. Wateja .
Baada ya kuona ni eneo gani linafaa kufanya biashara jambo la pili la kujiuliza je wateja wako watakuwa ni wakina nani? Hili ni swali la msingi sana kujiuliza kwa sababu lengo la kufanya biashara ni kupata wateja wengi, hata hivyo katika kuangalia hili pia fanya uchunguzi wa kina juu mahitaji ya wateja.

Hii utakusadia wewe pindi unapofikiri ni biashara gani ya kufanya.Tukiangalia tena mfano wa kuanziasha biashara ya vifaa vya shule yaani (stationery) tunaona ya kuwa wateja wako watakuwa ni wanafunzi na baadhi ya watu wengine kama eneo ambalo ulilifikiri la kufanyia biashara itakuwa kwenye taasisi yeyote mfano shule au kanisani.

3. Bidhaa.
Ewe msomaji wa makala hii unayependa kufanya biashara yeyote eidha ni ndogo au kubwa lazima ufikiri kwa kina je bidhaa gani ambazo utaziuza? Swali hili la bidhaa utajiuliza baada ya kufanya uchunguzi juu ya eneo husika la kufanyia biashara? na pia kwa kuangalia je ni mahitaji gani ya wateja ?

Pia jifunze kuangalia bidhaa ambazo baada yakufanya  uchunguzi na ukagundua ni bidhaa gani adimu pia zina uhitaji mkubwa chukua kama changamoto na lifanye kama fursa. Ukishapata majibu fanya utaratibu wote mpaka upate bidhaa hizo.

4. Matangazo.
Kuna usemi husema biashara matangazo. Hii ni kweli kabisa ili biashara iweze kuwa nzuri ni lazima wateja wako waipate kupitia matangangazo. Matangazo haya yanaweza kuwa kuwajulisha wateja wako juu ya ujio wa bidhaa mpya, mabadiliko ya bei na vitu vinginevyo vihusuvyo biashara.

Matangazo haya unaweza kuyasambaza kupitia mitandao ya jamii na vyombo vya habari pia kwa mfanyabiashara mdogo unaweza ukaandika bango  la biashara nje ya eneo lako la biashara unayoifanyia ili kuwajulisha wateja wako.