Mkurugenzi afunguka alivyopigiwa simu na Dkt. Mengi


Na Ferdinand Shayo-Kilimanjaro

Mkurugenzi wa Chuo cha St.Jose Training Trust,  David Dominic ameeleza mara ya kwanza alivyopigiwa simu na Dkt. Reginald Mengi ambaye alitoa ufadhili wa mwanafunzi kusoma katika chuo hicho.

Kwa Majonzi makubwa ameeleza kusikitishwa na kifo cha Dkt. Mengi ambaye alimpigia simu miaka mine iliyopita akiuliza kuhusu fani wanazozitoa, utaratibu wa kujiunga na malipo ambapo alimfadhili mwanafunzi mmoja kusoma chuoni hapo.
“Nakumbuka nilipigiwa simu tukazungumza nakihisi ni sauti yake hivyo nikamuuliza naongea na Mengi akasema ndo mimi, baada ya kuongea aliniagiza kwenda Bonite kuonana na Dada Mmoja anayefahamika kama Joyce ambaye alifanya malipo yote kwa maelekezo ya Dr.Mengi” alisema Mkurugenzi huyo.

Anasema kuwa alipata huzuni kubwa na masikitiko baada ya kusikia taarifa ya kifo chake kwani Mengi ana mchango katika chuo hicho.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia