Mahakama ya mwanzo Bukoba imemkuta na kesi ya kujibu mwandishi wa ITV Mkoani Kagera Audax Mutiganzi kwa kosa la kushambulia na kudhuru mwili.
Mwandishi huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 20,2019 katika maeneo ya mtaa wa Kashenye kwa kumshambulia Phinias Bashaya ambaye ni mlalamikaji.
Baada ya mahakama kusikiliza maelezo ya mashahidi wawili wa upande wa mlalamikaji hakimu wa mahakama hiyo Erick Ikera amesema Audax Mutiganzi ana kesi ya kujibu.
Shahidi wa kwanza ameieleza mahakama hiyo jinsi mshitakiwa alivyomshambulia mlalamikaji aliyekuwa amekaa pamoja na watu wengine nje ya duka maeneo ya mtaa wa Kashenye.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 255 ya mwaka 2019,mshitakiwa alidai kesi hiyo imefunguliwa sababu ya chuki dhidi yake na baada ya kukutwa na kesi ya kujibu ataanza kujitetea Mei 14 mwaka huu.
