Mwandishi ITV akiri kuendesha Gari bila leseni zaidi ya miaka mitano


Na. Clavery Christian, Bukoba

Mwandishi wa ITV Mkoani Kagera Audax Mutiganzi amejitetea leo katika shitaka la kushambulia na kudhuru mwili na kukiri kwa zaidi ya miaka mitano anaendesha gari bila leseni.

Kesi hiyo imeendelea leo katika mahakama ya mwanzo Bukoba na inasikilizwa na hakimu Erick Ikera na katika utetezi wake mshitakiwa alileta mashahidi wawili.

Mlalakikaji katika kesi hiyo Phinias Bashaya alimuuliza kama mshitakiwa ana leseni ya kuendesha gari ambapo alisema hakuwa na leseni.

Baada ya kukiri kuendesha gari bila leseni kwa zaidi ya miaka mitano mlalamikaji alimuuliza kwa jeuri hiyo anakosaje ujasiri wa kushambulia mtu kwa lengo la kumdhuru akijua kuwa hawezi kuchukuliwa hatua.

Mshitakiwa amesisitiza kuwa hakuwahi kumshambulia mlalamikaji huku akieleza mahakama kuwa siku ya tukio alipiga"Push up" 15 kama njia ya kujihami na mashambulizi ambayo yangetokea.

Hata hivyo mashahidi wake wawili Hermani Romward na Elieza Raphael walikana kumuona Audax Mutiganzi akipiga 'push up' na kuwa ndiye alichokozwa na mlalamikaji kwa kumdhalilisha kwa maneno.

Akijibu swali la mlalamikaji kwa nini hakuchukua hatua za kisheria kama alidhalilishwa kwa kutukana,Audax alidai kuwa ana kazi nyingi za kufanya na hakuwa na muda wa kupoteza kufungua malalamiko.

Kesi hiyo ya jinai namba 255/2019 baada ya hakimu kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili amesema hukumu itasomwa tarehe 28,May,2019 katika mahakama hiyo

Mpya zaidi Nzee zaidi