F Rais Magufuli aweka maua makaburi ya mashujaa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Rais Magufuli aweka maua makaburi ya mashujaa


Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo amekwenda kuweka shada la maua kwenye eneo la mashujaa waliopigania ukombozi wa Namibia.

Rais Magufuli amekwenda kwenye eneo hilo nje kidogo ya jiji la Windhoek akiwa amefuatana na mwenyeji wake Rais Hage Geingob.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa, kwenye eneo hilo wamezikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia wakiwemo waliopata mafunzo kwenye kambi ya Kongwa nchini Tanzania.

"Wengine walikuwa maafisa wa chama cha SWAPO ambao ofisi zao zilikuwa jijini Dar es Salaam na wengine ni viongozi wakuu walioendesha mapambano wakiwa nchini Namibia,"meeleza taarifa hiyo.