Simba SC wapata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC


Timu ya Simba SC leo wamebeba pointi tatu mbele ya Ndanda FC na kuanza kunukia ubingwa wa ligi msimu huu kwa ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Uhuru.

Ushindi huo umewapa nafasi Simba kujikita kileleni wakiwa na jumla ya pointi 88 na wamebakiwa na michezo mitatu ili kukamilisha mzunguko wa pili.

Kwa nafasi ambayo kwa sasa Simba wamefikia wanahitaji pointi mbili ili kujihakikishia kutetea ubingwa wao msimu huu, Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Singida United utakaochezwa Uwanja wa Namfua Mei 21.