Sudan Kusini kutumia Dola Milioni 3.2 kutibu wanajeshi wake


Sudan Kusini imetenga dola milioni 3.2 kutibu maafisa wa jeshi 281 waliojeruhiwa kwenye mapigano ambayo yamekuwa yakiendela nchini humo kwa miaka mitano.

Waziri wa habari Michael Makuei Lueth, amesema kuwa fedha hizo zitatumika kutibu wanajeshi waliojeruhiwa ambao hawajaweza kupata matibabu kwa sababu ya ukosefu wa pesa.