Na James Timber, Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Dola limefanikiwa kuwakamata na kuwashikilia watuhumiwa 29 kwa makosa mbalimbali yakiwemo mauaji, wizi wa majini kwa kutumia silaha na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Muliro Muliro amesema kuwa katika operation iliyofanywa na jeshi hilo ikiongozwa na taarifa za kiintelejensia wilayani ukerewe katika kisiwa cha Ukara walifanikiwa kuwakamata watu wawili kwa tuhuma za mauaji ambapo Machi 8, mwaka huu Majira 23:00 watuhumiwa hao waliwakamata na kuwafunga kamba kisha kuwatumbukiza majini majini wavuvi wawili kwa lengo la kuwapotezea maisha, ambapo mmoja alifariki dunia na mwingine alinusurika.
Kamanda ameeleza kuwa ufuatiliaji wa polisi kwa kushirikiana na raia wema ulifanikisha kuwakamata watuhumiwa hao waliofanya kitendo hicho cha kikatili.
Kamanda Muliro amesema kuwa Machi 20, 2019, Majira ya 22:00 jeshi la polisi lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa watano kwa kosa la kupatikana na vifaa vya kutengenezea noti bandia ambavyo ni karatasi zilizofungwa kwa nailoni na kuzungushiwa soltep zikiwa katika mabinda manne chupa ndogo nne na soltep moja, wakiwa na lengo la kuwatapeli wananchi kuwa wanauwezo wa kutengeneza pesa na kuwatajirisha watu.
Katika hatua nyingine Machi 14, mwaka huu Majira ya 10:30 asubuhi Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani hapa wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aliyefahamika kwa jina la Kibemba Warioba (27) askari magereza mwenye NO B.9205 WDR Biharamulo, akiwa na simu tano za aina tofauti zenye laini saba zilizosajiliwa kwa majina tofauti na mitandao tofauti kwa kujihusisha na makosa ya kujipatia pesa kwanjia ya udanganyifu, huku akitumia njia ya mitandao ya simu ambapo alianzisha SACCOSS fake iliyoitwa kwa jina la INFO TELL CCM akilenga kuwatapeli wanachama wa CCM na wengine katika mikoa ya Kagera na Mwanza kuwa "ukijiunga ni rahisi kupata gawio zuri na maisha yako ni rahisi kuwa bora"
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linatoa onyo kwa wananchi wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kuwa waache mara moja kwani ni kinyume na sheria na endapo mtu/watu watabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwani watakuwa wamejikatia tiketi ya kuwa kwenye msuguano mkali wa kisheria.