Anayedaiwa kumuua mwanafunzi wa chuo cha Kampala adakwa na Jeshi la Polisi


Kamanda wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Jeshi la Polisi  limefanikiwa kumkamata Ernest Joseph (19) kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Mgaya aliyefariki dunia Juni 17 baada ya kuchomwa kisu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Kamanda wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya Madale jijini hapa.

“Mtuhumiwa katika mahojiano na Jeshi la Polisi amekiri kumchoma kisu kilichosababisha kifo cha mwanafunzi huyo huku akieleza namna mwanafunzi huyo alivyokuwa amevaa siku hiyo ya tukio kuwa ni T-Shirt nyeusi, suruali ya Jinsi na Kapelo nyeusi.

“Aidha mtuhumiwa alikiri kumpora pochi iliyokuwa na simu moja aina ya Tecno rangi nyeusi,  fedha taslimu Sh 8,000 na vitambulisho mbalimbali ambavyo alivitupa na simu hiyo kuiuza,”amesema.

Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items