Argentina yaanza kwa kichapo Copa America


Timu ya Taifa ya Argentina imeanza vibaya michuano ya Copa America baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Colombia.

Magoli ya Colombia yalifungwa na Roger Martinez dakika ya 71 na la pili likifungwa na Duvan Zapata dakika ya 86.