Klabu ya Aston Villa imemuongezea mkataba kocha wake msaidizi, John Terry ambapo atasalia klabuni hapo hadi 2021.
Beki huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Chelsea amekua kocha msaidizi kwenye klabu hiyo kufuatia kuchaguliwa kwa Dean Smith kuwa kocha mkuu wa Aston Villa.