Klabu ya Azam FC imetangaza wachezaji ambao haitokuwa nao msimu ujao ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya msimu unaokuja.
Afisa habari wa Azam FC, Jafar Idd amesema timu hiyo inatarajia kuanza mazoezi hivi karibuni kujiandaa na michuano ya Kagame Cup..
.
"Wakati tukiendelea kujiandaa kuanza mazoezi, uongozi wa juu leo umenitumia majina ya wachezaji ambao mikataba yao imekwisha lakini baada ya mikataba yao kwisha klabu haitaendelea nao tena"-Jafar Idd Maganga.
.
Wachezaji hao ni
1. Joseph Kimwaga
2. Danny Lyanga
3. Hassan Mwasapili
4. Tafadzwa Kutinyu
5. Enock Atta Agyei
6. Stephan Kingue
7. Obrey Chirwa
8. Ramadhani Singano 'Messi'
Mikataba yao imekwisha na uongozi umewapa ruhusa ya kuondoka wakiwa wachezaji huru na kuangalia maisha mengine ya soka.

