Treni inayofanya safari zake toka Tabora -Dar imepata ajali Jijini Dodoma kabla ya kuingia stesheni, taarifa za awali zinadai kuwa Lori limegonga treni na mabehewa matatu ya daraja la tatu kitu kilichosababisha kupinduka na kuleta majera kwa baadhi ya Abiria.
Hadi sasa inaelezwa kuwa takribani watu 29 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ambayo inaelezwa kuwa ilitokea jana saa 5.30 usiku.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Protas Katambi ametoa maagizo kadhaa ikiwemo kumsaka dereva wa lori ambaye inasemekana aliruka kutoka kwenye lori baada ya ajali hiyo.
