Faida za kutumia nyanya chungu




Wengi tumekuwa tukitumia kama mboga au kiungo kimoja wapo katika kunogesha au kuongeza radha katika mboga lakini wachache mno wanaojua faida za nyanya chungu kiafya.

Pamoja na kufanya mboga kuwa na ladha na harufu ya aina yake, nyanya chungu zina kazi kubwa katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kujenga na kuimarisha afya ya mlaji.

Nyanya chungu ipo kwenye kundi la mbogamboga zenye virutubisho vingi ikiwemo vitamin A, B, na C ambazo zote kwa pamoja hufanya kazi ya kuboresha afya ya mwili kwa ujumla.

Nyanya chungu pia husaidia kuimarisha kinga ya mwilli na kumsaidia mlaji kuepukana na magonjwa ya mara kwa mara.

Nyanya chungu hizi ni kinga inayoweza kumwepusha mlaji kupata maradhi ya moyo. Kwa wagonjwa wa kisukari nyanya chungu pia ni dawa inayoweza kusaidia katika kupunguza kiwango cha sukari ndani ya mwili.

Vitamin K inayopatikana ndani ya nyanya chungu inasaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu.

Licha ya kuwa karibu, asilimia 90 ya nyanya chugu ni maji mboga hii pia inajumuisha madini ya chuma na potassium.

Hivyo kula nyanya chungu kwa wingi ili uweze kujitibu na kujibonya magonjwa mbalimbali.