Jeshi la Sudan lakiri ukiukwaji wa sheria

Jeshi linalotawala Sudan limekiri kwamba vikosi vya usalama vilikiuka sheria wakati vilipokuwa vikiwatawanya waandamanaji nje ya makao makuu ya kijeshi mji mkuu wa Khartoum wiki iliyopita.

Msemaji wa baraza la kijeshi la umpito, Jenerali Shams Eddin Kabashi, aliwaambia waandishi habari hapo jana kuwa uchunguzi unaendelea na kwamba maafisa kadhaa wa kijeshi wamewekwa kizuizini kwa mdai ya kwenda kinyume na maelekezo ya viongozi wa kijeshi.

Kabashi hakufafanua zaidi juu ya ukikwaji huu alioueleza kuwa 'mchungu na wa kikatili'.Kulingana na waandaaji wa maandaman ya Sudan watu wapatao 100 wameuawa katika mji mkuu wa Khartoum wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama.

Waandamanaji pia wamesema zaidi ya miili 40 iliopolewa katika Mto Nile mjini Khartoum na kuchukuliwa na vikosi vya usalama.