Kila wakati kumbuka jambo hili katika safari yako ya mafanikio

Ukisikia neno kufanikiwa , katika akili yako  hivi kwa harakaharaka huwa kinakujia nini? Maana watu wengi tumekuwa hatafahamu juu ya neno kufanikiwa. Wengi wetu hudhani ya kwamba neno kufanikiwa ni mafanikio yako binafsi tu, hivyo ndivyo ambavyo wengi wetu hudhani.

Huko ni kujidanganya, lakini ukweli ni kwamba ili yaitwe mafanikio ni lazima kufanikiwa kwako kuwe na matokeo chanya na  kwa watu wengine pia, huwezi sema umefanikiwa kama jamii na watu wengine waliokuzunguka wakiwa bado katika shida, hayo siyo mafanikio.

Ila mafanikio ni ile hali ya wewe  kuweza kuwasaidia watu wengine pia, huko ndiko tunakosema kufanikiwa. Wengi wetu tumekuwa wabinafsi sana katika mambo yetu mbalimbali tunayoyajua, tumekuwa tukiyona mafanikio katika maisha yetu tu, lakini ukweli ni kwamba kufanya hivyo si sawa hata chembe.

Kufanikiwa ni lazima kuwe na mahusiano ya wazi baina yako na watu wengine. Jaribu kuchukua dakika chache kisha uwaze je watu wengine wamekuwa wakinufaika nini kutoka kwako? Usinipe jibu. Kwa maana majibu unayo wewe.

Ila naomba nikusisitize kwa kusema ya kwamba jijingee nafasi ya kuwasaidia wengine kama unataka kufanikiwa zaidi, kwani unapofanya hivyo, ndivyo ambavyo unavyopata Baraka za kimafaniko zaidi. Kwani katika hili kuna usemi ambao husema anayetoa ndiye anayepokea zaidi.

Hivyo kila wakati jijengee uwezo ndani yako kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine haijalishi ni hali gani ambayo unayo. Najua  hapo bado njia panda kwamba nazungumzia nini? Usiajali nipo kwa ajili yako.

Ninachotaka kukwambia ni hivi jamii inayokuzunguka ni lazima inufaike kupitia wewe, nawe utanufaika zaidi kupitia jamii hiyo. Huwezi kusema unataka kufanikiwa wakati hauna mahusiano mazuri na watu wengine.

Hivyo kila wakati kama kweli unataka kufanikiwa jitahidi kuwasaidia watu wengine kwa kutoa mchango wako, ili siku moja watu hao waje watamke kwa vinywa vyao kwamba mafanikio yangu yamechngiwa na mtu fulani.

Pia kabl asijahitimisha kufanikiwa huenda sambamba na utoaji wa sadaka. kwani kuna mahali niliwahi soma, mwandishi alisema ya kwamba kutoa sadaka ni kumkopesha mwenyezi Mungu, huwezi kusema hufanikiwi wakati hutoi sadaka kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine. Hivyo kila wakati kama unataka kufanikiwa zaidi jitahidi kutoa sadaka kadri uwezavyo.  Na daima ili uweze kufanikiwa yakumbuke maneno haya ya kwamba mkono unatoa zaidi ndiyo mkono upokea mara dufu.

Hivyo jijengee mazoea ya kutoa sadaka na kuwapa mawazo watu wengine ambayo yatawajenga kwa namna moja ama nyinyine. Hivyo ni vyema ukafikiria na kuona na kwa jinsi gani unavyoweza kuinufaisha jamii yako kwa hicho kidogo ilichonacho.

Mpaka kufikia hapo ndugu yangu sina jambo la ziada la kusema  zaidi ila hakikisha ya kwamba unakuwa ngao zaidi kwa  watu wengine kwa kutoa mchango wako kwa namna moja ama nyingine.  Nikiutakie siku njema na utekelezaji mwema.

Na. Benson Chonya