Loading...

6/14/2019

Klabu ya Brighton ya Uingereza yataka kumsajili kapteni wa Mbwana Samatta


Klabu ya Brighton ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Genk juu ya kumsajili wa captain wa klabu hiyo ya Ubelgiji Leandro Trossard.

Winga huyo 24 ambaye amefunga magoli 22 kwenye mashindano yote ya mabingwa hao wa Ubelgiji msimu uliopita pia wamecheza mara sita Europa League.

Ofa ya kwanza ya Brighton ilikataliwa mapema wiki hii lakini mazungumzo baina ya vilabu hivyo yanaendelea.

Taarifa zinsema klabu ya Genk wanataka kiasi £17.8m ambacho kitakua kimezidi kiasi kilichoweka rekodi klabuni Brighton cha £17m walicholipa kwa Alireza Jahanbakhsh majira ya kiangazi yaliopita.
Loading...