Mbunge asimulia alivyouza mboga akiwa Chuoni



Na John Walter-Manyara

Wanawake mkoa wa Manyara wametakiwa kuto kukata tama katika utafutaji ili kutimiza ndoto za maisha yao.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge viti Maalum Mkoa wa Manyara Ester Mahawe akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati alisema kuwa hakunamaisha yeyote yanayokuja kirahisi bila kupitia changamoto.

Mahawe alisema kuwa mpaka kufikia hatua ya kuwa Mbunge amepambana na mapito mengi ikiwa ni pamoja na ujasiriamali mdogo [Machinga].

“Nilikuwa nikiuza mboga za majani aina ya chainizi nikizitoa Mbulu kuzipeleka Singida na wakati Mwingine mboga zikiwa adimu nabadilisha biashara napeleka Mayai” alisema Mahawe.

Mahawe aliongeza kwa kuwaasa na kuwapa Moyo wanawake wote wenye uthubutu wa kujituma katika kutafuta maisha.