'Mwanaume ashikiliwa kwenye Gereza la wanawake'


Kulikuwa na hali ya mshtuko katika mahakama moja mjini Eldoret siku ya Jumanne baada ya kubainika kuwa mshtakiwa aliyekuwa akishikiliwa kwenye gereza la wanawake ni mwanaume.

Mshtakiwa huyo anayetambulika kwa jina Shieys Chepkosgei siku ya Jumatatu alikamatwa katika Chuo na Hospitali ya Rufaa ya Moi ambapo alikua akifanya kazi kama muuguzi mwanafunzi wa kike ingawa hakusajiliwa hapo.

Baada ya kushtakiwa, alipelekwa kwenye gereza la wanawake la Eldoret kusubiri maamuzi ya mahakama huku akitambuliwa kama mwanamke, Gazeti la Daily Nation la Kenya limeripoti.

Hatahivyo, siku ya Jumanne askari magereza katika ukaguzi wao wa kawaida waligundua kuwa mshtakiwa alikua mwanaume.

Uchunguzi wa haraka ulifanyika kubaini ukweli kabla ya kufanyiwa vipimo ili kujihakikishia jinsia yake.

Hakimu wa mahakama hiyo, Charles Obulutsa siku ya Jumanne alilazimika kutoa amri nyingine ikielekeza kuwa mshtakiwa ashikiliwe kwenye kituo cha polisi cha Eldoret Magharibi ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi wa kitabibu kuthibitisha jinsia yake.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items