Watu watano wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya makundi mawili kugombani ndani ya hospitali katika wilaya ya Nankana Sahib ya jimbo la Punjab mashariki mwa Pakistan.
Kulingana na ripoti hiyo ya vyombo vya habari, makundi hayo mawili kutoka ukoo tofauti yalifyatuliana risasi Jumatatu baada ya mgogoro mdogo katika sehemu ya dharura.
Baada ya majibizano hayo ya risasi yalisababisha vifo vya watu wanne papo hapo na wakijeruhi wengine kadhaa, mmoja alikuja kufariki hapo baadaye.
