Rais Putin huenda akakutana na Trump nchini Japan

Ikulu ya Urusi imearifu leo kwamba Rais Vladmir Putin na mwenzake wa Marekani Donald Trump huenda wakakutana kwa muda mfupi katika mkutano wa kundi la nchi tajiri kiviwanda na zile zinazoinukia kiuchumi la G20 utakaofanyika nchini Japan wiki ijayo.

Msemaji wa Putin,Dmitry Peskov amewaambia waandishi habari kwamba viongozi hao hawatokuwa na mkutano kamili watakapokutana kwenye mkutano huo wa kilele utakaofanyika mjini Osaka kuanzia Juni 28.

Wiki iliyopita Trump alisema atakutana na Putin pembezoni mwa mkutano huo wa Japan lakini alitaka mkutano huo uhudhuriwe pia na watu wengine kwasababu waandishi wa habari hawana wanachokiamini.

Wakati huohuo Trump binafsi anajiandaa kesho Jumanne kutangaza rasmi nia yake ya kutaka kugombea tena urais katika uchaguzi wa 2020 nchini Marekani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia