Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi kuzuru Tanzania


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi anatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi, Juni 13 kwa ziara ya siku mbili.

Rais Tshisekedi alichaguliwa mapema mwaka huu akichukua nafasi ya Joseph Kabila aliyeongoza nchi hiyo kwa miongo kadhaa.

Felix Tshisekedi aliapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo January 24.2019 katika hatua ya kwanza ya kihistoria tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960.