Rais wa DRC amaliza ziara yake Tanzania


Rais Felix Antoine Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokradia ya Kongo (DRC) amemaliza Ziara yake ya Kitaifa ya siku mbili nchini.

Rais Felix ameagwa na Rais Magufuli katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuelekea nchini Burundi.

Rais Felix aliwasili nchini siku ya jana kwaajili ya ziara yake ya kikazi.