SMZ yashauriwa kufanya ukarabati wa barabara zilizoharibika


Na Thabit Hamidu, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshauriwa kuzifanyia ukarabati na matengenezo barabara zilizo athiriwa na ujenzi wa mitaro ya maji ya Mvua inayoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali ndani ya mji wa Zanzibar.

Ushauri umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Baraza la wawakilishi ya Adhi na Mawasiliano Hamza Hassan Juma  wakati wakiwasilisha  ripoti ya kamati yao katika kikao hicho cha baraza la wawakilishi Ckuwani Nje ya Mji wa Zanzibar.

Mwenyekiti Hamza alisema Serikali ya Mapinduzi inapaswa kuhakikisha kuwa inazifanyia  ukarabati  barabara zilizoathiriwa na ujenzi wa mitaro ya maji ya Mvua inayoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuondoa usumbufu ambao unajitokeza kwa wananchi mbalimbali ambao wanatumia barabara hizo.

“Kiukweli katika maeneo ambayo kumepitishwa mitaro hiyii ya maji ya mvua kumekuwa na usumbufu kwa wananchi hivyo niwaombe serikali yetu tukufu kujitahidi katika kuzifanyia ukarabati na kuondoa usumbufu kwa wananchi wetu hususani abiria na madereva wa daladala wakiwa Safari” alieleza Mwenyekiti huyo.

Aliongeza kuwa ukarabati wa Barabara hizo kutaweza kurahisha huduma za usafiri pamoja na kuwapunguzia usumbufu wananchi kutokana na ubovu wa barabara.

Hata hivyo Hamza alisema  miongoni mwa Barabara hizo ni pamoja na Barabara ya Mikunguni,Shaurimoyo pamoja na Chukwani ambapo zinaleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji hususan wakati wa mvua na kusababisha msongamano wa Gari.

Katika maelezo yake alisema serikali itakapo zifanyia Marekebisho kwa wakati itasaidia upatikanaji wa huduma ya usafiri inayozingatia sheria za na Usalama wa barabarani.

Katika hatua nyingine alisema suala la Ununuzi wa Mtambo mpya wa Lami pamoja na Vifaa vya ujenzi wa Barabara Mwenyekiti huyo amesema ni vyema kwa idara ya utunzaji wa Barabara kuwapa elimu ya kutosha watendaji wake ili waweze kutumia vifaa hivyo kwa ufanisi.

Alisema  Mtambo wa lami unahitaji utaalamu katika matumizi yake hivyo ni vyema kwa watendaji kupewa elimu kabla ya kutumia mtambo huo.