Tani Milioni 1 za ufuta zanunuliwa, DC atoa neno kwa wakulima


Na Ahmad Mmow-Nachingwea

Jumla ya tani 1,884,000 za ufuta zimenunuliwa kupitia chama kikuu cha ushirika cha RUNALI mkoa wa Lindi. Katika mnada huo uliofanyika jana katika kijiji cha Mbondo, tarafa ya Kilimarondo, wilaya ya Nachingwea bei ya juu ilikuwa shilingi 2,860 na bei ya chini shilingi 2,852 kwa kila kilo moja.

Mnada huu ni wakwanza kufanyika kupitia chama kikuu cha ushirika cha RUNALI katika msimu huu wa 2018\2019. Mnada wa kwanza katika chama cha RUNALI kinachoundwa na vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) ulitara

Wakati huo mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango licha ya kuwashukuru wakulima hao wa ufuta kukubali kuuza kwa bei hizo, lakini pia aliwataahadharisha kuhusu madhara ya kugomea bei.

''Mwaka jana kulifanyika mgomo ambao wakulima wengine walifuata mkumbo tu. Hata hivyo matokeo yake yalikuwa kama mtego wa panya,'' alisema Muwango.

Muwango alifafanua kwamba madhara ya mgomo huo yameathiri vyama vya msingi, vyama vikuu vya ushirika, serikali kuu, halmashauri na baadhi ya wakulima. Kwa hiyo kabla ya kushiriki migomo waanze kufikiria madhara yanayoweza kusababishwa na migomo hiyo.