Loading...

6/15/2019

Uwanja wa kisasa uliojengwa Mwanza, Simba SC na Gwambina FC kucheza mechi ya ufunguzi


Kufuatia kumalizika kwa msimu wa ligi kuu Tanzania bara na kusubiri musimu ujao wadau mbalimbali katika kuendeleza soka nchini wameendelea kuboresha michezo nchini kwa kusajili wachezaji wapya na kuboresha miundombinu ya viwanja.


Kupitia mpira wadau wa mpira wilaya ya Misungwi mkoani mwanza wameamua kujenga uwanja mpya wa kisasa zaidi ambao uko nje kidogo na jijini la Mwanza wenye uwezo wa kubeba zaidi ya watazamaji elfu kumi na moja.

Akizungumzia kuhusu ujenzi huo ambao uko katika hatua ya mwisho  meneja wa ujenzi Bw.Nyanda Mnyeti amesema kuwa walianza ujenzi kwa na mkandarasi mwingine ambaye alizungushia tofali na baadae wakapata mkandarasi mwingine ambaye alichimba na kuweka udongo ambayo unaofaa kwa ujenzi kama tofauti na awali.

Ameongeza kuwa uwanja huuo ni wa kisasa kwani ujenzi wa uwanja huo wamejifunza kupitia viwanja vya nje ya nchi ambapo maegesho ya magari yatakuwa nje wakati wa mechi huku makazi ya  kocha,Viongozi na wachezaji watakuwa wanaishi karibu na uwanja ambapo kuna nyumba (Hostel) zao tayari za kuishi.

Kwa upande wake katibu wa timu ya Gwambina Fc Bw.Donald Kilai amesema kuwa ifikapo tarehe 21 Juni uwanja utafunguliwa kwa mechi kali kati ya Gwambina Fc na Simba Sc ya Dar es Salaam huku kukianziwa na sala na michezo mbalimbali siku hiyo.
Kwa upande wa usalama Donald Kilai amesema kuwa hali ya usalama kwa kushirikiana na jeshi la polisi utakuwa salama hakuna tatizo kila kitu kimeandalia.

Kwa upande wa mashabiki na kiingilia Kilai amesema kuwa  kutakuwepo na gharama ya kiingilio huku akitaja sehemu ambapo tiketi zitauzwa kwa gharama nafuu ni pamoja na jijini Mwanza, Misungwi mjini na uwanjani ambapo kutakuwepo na magari ambayo yatakuwa yanazunguka na kuuza tiketi hizo.

Loading...