Wachezaji wa zamani wapatiwa tiketi za kwenda Misri


Na Thabit Hamidu,Zanzibar

TAASISI ya Mimi na Wewe imewafadhili wachezaji wawili wa zamani wa timu ya taifa akiwemo Seif Nassor Bausi na Othman Abdull Ali kwenda Misri kwa ajili ya kuhamasisha timu ya Taifa katika fainali za Afrocon.

Wachezaji hao wa zamani wa timu ya taifa wanatarajiwa kusafiri nchini Misri kwa siku 10 ambapo wanatarajia kuondoka Juni 21 mwaka huu kwa ajili ya kuhamasisha timu ya Taifa katika michuano hiyo.

Akikabithi fedha taslimu mbele ya Rais wa Zanzibar Fortball  Federation(ZFF),Seif Kombo kwa wachezaji hao wa zamani Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ayoub Mohamed Mahoumud alisema hatua hiyo ya kuwapeleka wachezaji hao ni sehemu ya humasishaji wa timu ya taifa kwa upande wa Zanzibar.

Mwenyekiti huyo alisema taasisi yake imeona kufanya hivyo ni kuhamasisha watanzania katika kuhakikisha timu ya taifa inapata ushindi kwenye michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Misri.
Alisema taasisi hiyo inagharamia usafiri,malazi na hudhurihaji wa mechi katika viwanja hivyo ambavyo timu ya taifa itakuwa inacheza ambapo alitaja zaidi ya sh.milioni 7 zitagharimu kwa wachezaji hao.

"Hii ni hatua kubwa katika kuwatia moyo wachezaji wetu na ndio mchango wetu kwa Zanzibar katika kuhamasisha timu yetu ya taifa inapata ushindi na pia kitendo hichi ni ishara nzuri ya kuona Zanzibar inafanya mageuzi ya mpira kwa namna hii,"alisema Mwenyekiti huyo

Naye Rais wa ZFF,Seif Kombo alisema wachezaji hao watapelekwa Misri katika kuona na kutia moyo timu ya taifa kwenye michuano ya Africon 2019.

Alisema pia kitendo hicho ni ishara ya kuwafariji na kuwathamini wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya kutambua mchango wao mkubwa walioutoa kwenye kipindi chao cha kuitumikia timu ya taifa.

"Najua hata wengine watapata faraja ya kuona kumbe wachezaji wa zamani wanafarijiwa na hivyo wachezaji wa sasa ambao ni vijana watapata moyo wa kuendelea na mpira kwa kuona kitendo hichi cha kufarijiwa," alisema

Kwa upande wake Seif Nassor Bausi ambaye ni miongoni mwa wachezaji hao wazamani ambao wanatarajia kwenda kuhamasisha timu hiyo ya taifa alitoa shukrani zake kwa tukio hilo na kwamba kitendo hicho kina ashiria kuthaminiwa kwa michango yao katika kipindi chao.

Alisema mbali na hilo pia kitendo hicho kinatoa hamasa kwa timu za ndani kuwathamini wachezaji mbalimbali wa zamani na kwamba pongezi kubwa ziende kwa taasisi hiyo ya Mimi na Wewe kwa mchango wao.

Naye Othman Abdull Ali ambaye pia ni mchezaji wa zamani atakaye kwenda huko kuhamasisha timu ya taifa ambapo alisema kitendo hicho ni mshangao mkubwa kwake kwa kupata fursa hiyo na kwamba ni ishara ya kuthaminiwa kwa mchango wake.

"Nimeshangazwa sana nilikuwa nyumbani ghalfa nikapigiwa simu kuhusu jambo hili lakini ni mwanzo mzuri kwa jambo hili na kwamba ni mara ya kwanza kutokea Zanzibar,"alisema