Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya njombe Ally juma amewaagiza wasimamizi wa mradi wa kunusuru kaya masikini tasaf kwenda kuwasaidia walengwa kwa kuwaelekeza namna sahihi ya kutunza fedha wanazopatiwa ili ziweze kuwasaidia kwa lengo lililokusudiwa badala ya kuzifuja.
Agizo hilo analitoa wakati akifungua semina ya siku tano kwa maofisa wawezeshaji wa tasaf toka ngazi ya kata na halmashauri ambao watakwenda kuwasaidia wananchi hao namna ya kuzitunza fedha na kuzitumia kwa malengo kusudiwa baada ya kufunguliwa kwa vikundi vya akiba.
“ fedha hizi zinatolewa nyingi katika mradi wa tasaf lakini lengo halitafikiwa kama mtu hana elimu ya kusave,tuelimisha wananchi wetu ili fedha hii waweze kuitumia vizuri ili hata mradi huu hapo baadaye ukiisha wawe na shughuli zao za uchumi zitakazoendesha maisha yao ya kawaida”alisema Ally Juma
Shaban abdumalick ni kaimu meneja idara ya miundombinu tasaf makao makuu anasema ili kukamilika kwa mradi huo wa miaka mitano ni lazima walengwa wote wajiunge kwenye vikundi vya kuweka akiba.
“Haikuwa tu madhumuni yetu kuwapa ruzuku ya msingi na masharti na kuishia hapo,bali wafanye miradi wapate ajira ya muda lakini pia wajiunge na vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza ili wakamilishe lile zoezi zima la kuondoa umaskini”amesema Shabani
Baadhi ya washiriki toka katika kata mbalimbali ndani ya halmashauri ya wilaya ya njombe akiwemo Anold Luyoka ambaye ni afisa elimu kata ya Mfiriga na Tumain nziku ambaye ni afisa maendeleo ya jamii kata ya Mtwango wanakiri kuwa mradi wa tasaf umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi ambao hali yao ya maisha ni duni kwani kwa sasa wameonekana kuimarika kiuchumi kutokana na elimu wanayopata juu ya matumizi ya fedha wanazopata na ajira ndogo ndogo wanazopata.
Mradi wa tasaf kwa sasa umeonekana kuwa na mwitikio mkubwa katika jamii kutokana na walengwa wengi kuimarika kiuchumi kutokana na fedha ambazo wamekuwa wakipatiwa ambazo zimekuwa wakizitumia kwa kufanyia miradi kama ya ufugaji,kilimo pamoja na kusaidia familia zao katika mahitaji madogo madogo.

