Wanafunzi wa kidato cha sita kupatiwa mafunzo ya Ujasiriamali



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita katika shule mbalimbali wanatarajia kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali yatakayowawezesha kutambua fursa zilizowazunguka  pamoja na kujiajiri ili kupunguza tatizo la ajira miongoni mwa vijana.

Mkuu wa Idara ya Ushauri katika Chuo cha Uhasibu Arusha Pamela Chogo alisema kuwa wameamua kutoa mafunzo  kutokana  changamoto wanazoziona kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali pindi wanapohitimu masomo  yao.

Alisema mafunzo hayo ya ujasiriamali yatawasaidia kufanya maamuzi ya kijana katika maisha  na kuweza kujitambua ili waweze kujiajiri kutokana na  tatizo La soko  ajira lililopo nchini.

Mafunzo hayo  ni ya muda wa  wiki sita nayataanza  tarehe 10 mwezi wa sita yakilenga  kufundisha elimu mbali mbali ya ujasiriamali,namna ya kujitambua pamoja na  jinsi ya kuweza kuajiriwa.

"Ili kuhakikisha tunatoa elimu hiyo kwa undani zaidi tutawaalika wadau wa wataalamu wa SIDO kutoa elimu ya ujasiriamali pamoja na wataakamu wa mikoani kwaajili ya kutoa elimu ya mikopo  wataalamu wa Afya" alisema Pamela Kichogo.

Adha alisema katika kutoa elimu ya Afya  itawasaidia vijana katika Afya ya uzazi kwani vijana wengi hawaelewi Afya ya uzazi hivyo ulazimika kutafuta taarifa hizo kwenye mitandao  ambayo haina ukweli wa kile wanachokihitaji.

Mbali na hilo watatoa  elimu ya kujisimamia na jinsi ya kujilinda  kama kijana hususani kwa wale  waliohitimu elimu ya sekondari kwani vijana wengine  hawawezi kujilinda huku wengi wao wakiingia katika  makundi ya mitaani na kufanya uhalifu.

Hata hivyo vijana wametakiwa kuachana na dhana ya kubweteka na kulalamika lika siku kuwa kahuna ajila huku wa kitakiwa kuzingatia kuwa Tanzania ya Viwanda inawezekana na waanzilishi wa viwanda hivyo ni wao na siwengine.