Watu 12 wafariki katika tetemeko la ardhi China

Nchini China idadi ya vifo imeongezeka leo hadi watu 12 na wengine 134 wamejeruhiwa kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.0 katika vipimo vya Richter.

Zoezi la uokozi linaendelea huku waokoaji wakijaribu kuwatoa watu waliokwama chini ya majengo yaiyoporomoka.

Zaidi ya watu 4,000 walihamishwa kutoka makaazi yao kutokana na idadi kubwa ya majengo kuharibika au kuporomoka kabisa kufuatia tetemeko hilo la jana nje kidogo ya mji wa Yibin katika jimbo la Sichuan.

Matetemeko ya ardhi hupiga mara kwa mara katika jimbo la Sichuan, ambapo tetemeko kubwa la kipimo cha Richter 7.9 lilisababisha watu 87,000 kupoteza maisha yao au kutojulikana walipo mnamo mwaka 2008.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items