Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu matarajio ya ongezeko la watu duniani inaonyesha kuwa katika muda wa miaka 26 ijayo, kutakuwepo ongezeko la watu bilioni mbili.
Ripoti hiyo iliyotolewa jana, inasema ingawa nchi nyingi zinazidi kuwa na wakaazi wengi wa makamo, nchi chache zitashuhudia mpasuko mkubwa wa kuongezeka kwa watu wake.
Matazamio ya ripoti hiyo ni kwamba ifikapo mwaka 2050, nusu ya vijana duniani watakuwa wakiishi katika nchi za Nigeria, India, Pakistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Tanzania, Indonesia, Misri na Marekani.
Vile vile ripoti hiyo inatabiri kuwa mwaka 2027 India itakuwa imeipiku China kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya watu wa China itapungua kwa asilimia 2.2 kati ya mwaka huu wa 2019 na 2050.