Na James Timber, Mwanza
Mkazi Mmoja wa Kjiji cha Iligamba kitongoji cha Chang’ombe Kata ya Iligamba Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, Debora Benado (37) aliyepotea ndani ya siku Nne amekutwa ameuwawa na mwili wake kutupwa kichakani.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Chang’ombe Petro Chimini alisema kuwa mwili wa marehemu huyo umegundulika usiku wa kuamkia leo Majira ya 20:00 baada ya watoto waliokuwa wakicheza mpira kupita katika maeneo hayo na kusikia harufu kali kisha kutoa taarifa.
Mara baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kukuta mwili wa mama huyo ukiwa uchi wa mnyama ndipo walipotoa taarifa kituo cha polisi kwa lengo la kupata msaada.
"Tulipopata taarifa kutoka kwa watoto wacheza mpira tulifika eneo hilo ambalo linaumbali wa kilometa moja kutoka kwa marehemu huyo ili kubaini kuwa kunakitu gani tulipofika tukakuta ni mwili wa Debora Benado ukiwa umeharibika," alisema Chimini.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole alisema amekwisha pata taarifa ya juu ya tukio hilo na vyombo vya dora vinafanya uchunguzi juu ya tukio hilo na tayari linamshikiria aliyekuwa mume wa marehemu huyo Nzito Lukansola kwa mahojiano zaidi.
Kipole alisema mala uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama utakapo kamilika na madaktari kubaini kifo chake msako wa kuwasaka waliofanya tendo hilo utaanza na watafikishwa mahakani kwa mjibu wa sheria.
Tukio hili nilapili ndani ya miezi miwili ambapo Mei 25, mwaka huu Tumaini Faustini (35) mkazi wa kijiji cha Nyakahako Kata ya Chifunfu Wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza alinyongwa hadi kufa na mwili wake kukutwa umetundi juu ya mti.
"Matuki haya yananisikitisha sana jamii inatakiwa kuelewa kumudhuru binadamu mwenzako ni kosa na siyo uungwana na kila mwanadamu anahaki ya kuishi siyo kukatishwa maisha," alisema Kipole .
Baba mdogo wa marehemu huyo Emmanuel Masinde alisema kuwa alipata taarifa za binti yao kwa mshituko mkubwa na alikutana naye wiki moja kabla ya kifo chake.
Alisema hadi sasa familia inashangazwa na tukio hilo na binti yao alikuwa ametengana na mume wake kwa muda wa miaka miwili na tukio hili limezua simanzi kubwa ndani ya familia.
Masinde alisema mtoto wao ameacha watoto saba ambao familia imeachiwa jukumu la kuwatunza na kisha kuwalea pia naomba vyombo vya dora kuchunguza tukio hilo na watakao bainika wachukuliwe hatua za kisheria.
Onesmo Cristopha ni binamu wa marehemu alisema siku ya ijumaa iliyopita walikuwa pamoja wakivuna mpunga shambani mala baada ya kumaliza kuvuna mpunga alimuaga akimwambia kuwa akachimbe viazi shambani kwa ajili ya chakula cha watoto na hakuonana naye tena hadi usiku wa kuamkia leo alipokutwa amefariki.
