Afa maji akiokota samaki Ziwa Victoria



Na James Timber, Mwanza

Mkazi wa Kijiji cha Nyehunge Kata ya Nyehunge Wilayani Sengerema katika Mkoa wa Mwanza John Paul (23) amepoteza maisha akiokota samaki  ndani ya ziwa Victoria.

Tukio hilo limetokea jana Majira  ya 13:00 kwenye kisiwa cha Gembale kilichopo kijiji cha Kanyala Kata ya Bulyaheke Wilayani Sengerema.

Afisa Mtendaji Kijiji cha Kanyala  Benjamini Nhungwizi alisema marehemu huyo alikumbwa na mauti hayo wakati alipokuwa ndani ya ziwa akitumia mtumbwi mdogo wa kasia akiokota samakini waliokuwa wameibuka ndipo alipokumbwa na dhoruda chombo kikapinduka na kupoteza maisha.

Ikimbukwe kuwa mwezi Februari na Juni kila mwaka samaki aina ya sangara huibuka kutokana na joto chini maji hukimbia juu na jamii ya wavuvi hupata mavuno mengi kutokana na samaki hao kuibuka na kuwageuza kwa kitoweo.

"Wavuvi wengi waliingia ziwani kuokota samaki lakini hawa kuzama inasemekana alikuwa amelewa hivyo wanatakiwa wavuvi kuchukuwa tahadahari kabla ya kuingia ziwani endapo kama umetumia kilevi," alisema   Nhungwizi.

 Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole alisema anataarifa juu ya tukio hilo na kuwataka wavuvi kuchukuwa tahadhari wakati wanapokuwa ziwani wakivua samaki.

Mmoja wa wananchi waonaofanya shughuli za uvuvi kisiwa cha Gembale Hasan Mhenga alisema matukio mwengi ya namna hii hutokana na wavuvi kutokuwa makini hivyo jamii ya wavuvi wanapaswa kujitambua.

Baba wa marehemu huyo Khaji Paul alisema kuwa alipata taarifa za mtoto wake kufa maji jana Majira ya saa 8 mchana na mwili wa mwanaye unatarajia kuzikwa leo kijijini kwao Nyehunge.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items