Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa ebola ambao umeendelea kuwepo katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda.
Majaliwa alisema hayo jana wakati akiahirisha Mkutano wa 15 wa Bunge la Bajeti jijini Dodoma.
Alisema kutokana na mwingiliano wa nchi hizo, Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kukabiliana tishio la ugonjwa huo.
“Ugonjwa huu wa ebola umeendelea kuwepo Congo, umelipuka tena Uganda sote tunatambua upo mwingiliano wa nchi hizi, katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti.
“Lakini pia nitoe wito kwa Watanzania kuchukua hatua kutokana na hatari iliyopo katika ugonjwa huu,”alisema.
