Atakaye pambana na Rais Magufuli tutamshughulikia - RC Hapi


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, RC Ally Hapi amesema kuwa atakaye pambana na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli awatamshughulikia.

Hapi amesema kuwa  wale wote waliojipanga kupeleka mashambulizi kwa Rais tunawajua kwa majina tunawajua kwa mafile yao.

"Membe alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje ataweza leo hii amekuwa Mwananchi wa kawaida, kazi yetu ni kupambana na wakina Membe wa sasa na wanaokuja, atakaepambana na Rais wetu tutamshughulikia sisi wenyewe tutamalizana nae wale wote waliojipanga kupeleka mashambulizi kwa Rais tunawajua kwa majina tunawajua kwa mafile yao," amesema Hapi leo Mkoani Iringa katika mkutano wake na Waandishi wa habari.

Hata hivyo Hapi alisema "Wastaafu wakae kimya zama zao zimekwisha  mazuri waliyofanya tunawashukuru, popote watakapo jitokeza tutawatwanga hatutawaacha hivi hivi kamwe."