Beki wa klabu ya Tottenham Kieran Trippier, amekamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Atletico Madrid kwa dau la £20m.
Trippier mwenye miaka 28 alijiunga na Spurs akitokea Burnley mwaka 2015 na amecheza michezo zaidi ya 100 na klabu hiyo ya jijini London, amesaini mkataba wa miaka minne kwenye klabu ya Atletico Madrid.