F Njombe waitikia zoezi la upimaji wa afya Ikelu,Daktari Asema "Wengi Waliofika Kupima Wakutwa Na Presha" | Muungwana BLOG

Njombe waitikia zoezi la upimaji wa afya Ikelu,Daktari Asema "Wengi Waliofika Kupima Wakutwa Na Presha"











Zaidi ya watu 400 wamejitokeza kupata huduma ya vipimo vya afya bure katika hosptali ya St.Joseph Ikelu iliyopo mjini Makambako huku wengi wao wakibainika kuwa na magonjwa yasiyoambukizwa hasa kisukari,shinikizo la damu(Presha) na matatizo ya figo.
‎Akizungumza baada ya zoezi la utoaji vipimo bure  kuhitimishwa Septemba 19,2025 Daktari wa hospitali ya St.Joseph Ikelu Polycarp Nyengele amesema licha ya watu wengi kubainika na magonjwa hayo pia wamebaini uwepo wa wanawake ambao wanakabiliwa na changamoto za uzazi.

"Wengi sana wamekuja wakiwa na matatizo ya uzazi na wengine saratani ya shingo ya kizazi na hizi changamoto zina visababishi vingi"amesema Nyengela
‎Dkt.Polycarp Nyengele amesema magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wa maisha hasa ulaji wa vyakula huku akiitaka jamii kutengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kuzingatia ulaji wa vyakula.
‎Afisa maendeleo kata ya Utengule mjini Makambako Catherine Steven amesisitiza umuhimu wa  wananchi kuwa na afya imara ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi bila kikwazo.
‎Baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kupima afya zao,John Mlowe,Lida Tweve,Ambonise Mtivike na Edmund Mkongwa wametaka elimu kuendelea kwa jamii ili ipate mwitikio wa kupima afya zao kwa hiyari.
‎Zoezi la utoaji wa vipimo bure kwa wananchi katika hosptali ya St.Joseph Ikelu limefanyika kwa siku mbili kuanzia Septemba 18 hadi Septemba 19,2025 ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii faida ambayo hosptali hiyo imepata.

Post a Comment

0 Comments