https://monetag.com/?ref_id=TTIb Baada kufurushwa Simba SC, Mzee Kilomoni atema nyongo | Muungwana BLOG

Baada kufurushwa Simba SC, Mzee Kilomoni atema nyongo


Baada ya jana uongozi wa Simba SC kupitia kwa Mkurugenzi wake Crescentius Magori kusema kuwa haimtambui aliyekuwa mdhamini wa Klabu hiyo Mzee Hamisi Kilomoni kama mdhamini ndani ya Klabu hiyo tangu mwaka 2017 walipomvua wadhifa huo, Mzee huyo amejibu.

Kupitia E FM Radio leo Mzee Kilomoni amesema kuwa hawamtambui Magori ndani ya Klabu hiyo na bado anatambua nafasi yake pale pale.

"Magori ni nani ndani ya Simba SC? yeye anazungumza kama nani ndani ya Simba na anacheo gani?" Mzee Kilomoni

Mzee Kilomoni ameongeza kuwa huko alikoshitakiwa kwenye Kamati ya maadili ya TFF ndio atazungumza mambo mengi zaidi.

Kilomoni pia amesema kuwa wiki ijayo siku ya Jumatano atakuwa na mkutano wa mwanzo na mwisho wa kuzungumzia masuala haya. "Wiki ijayo jumatano nitakuwa na mkutano wa mwanzo na mwisho wa kuongelea haya mambo na utakuwa ni wamoto"