Loading...

7/11/2019

Bibi wa miaka 83 apatikana na hatia ya kuwa na bangi

Mwanamke mmoja mwenye miaka 83 aliyekutwa na gramu 600 za bangi amekutwa na hatia nchini Kenya, redio ya Capital fm imeripoti

Akiwa mbele ya hakimu mkazi Nelly Kariuki siku ya Alhamisi, Lydia Mumbi Ndirangu amekiri kuwa alikutwa na bangi ya thamani ya sh 500 za katika eneo la Muthinga, jimbo la Tetu.

Mtuhumiwa ataendelea kushikiliwa na kurudi tena mahakamani tarehe 15 mwezi Julai wakati atakaposomewa hukumu.

Hii ni kesi ya pili kuhusu mihadarati katika kipindi cha miezi miwili tu.

Mwezi Mei mwaka huu, mahakama ya Nyeri ilimhukumu mwanamke mmoja wa makamo, kifungo cha miaka 30 kwa makosa ya kusafirisha bangi ya thamani ya shilingi 2,820 bila faini .

Gazeti la daily Nation limesema kuwa inaaminika bibi huyo amekuwa akinunua bangi mjini Nyeri na kuipeleka kwa mtoto wake wa kiume ambaye huwauzia wateja.
Loading...