British Airways yasimamisha safari zake kwenda Misri


Shirika la ndege la British Airways limesimamisha safari zake za ndege kuenda mjini Cairo, Misri kwa muda wa siku saba.

Shirika hilo lilitangaza kwenye tovuti yake kwamba limechukua hatua hiyo ili kutathmini hali ya usalama, lakini halikutoa maelezo zaidi.

Hata hivyo taarifa nyingine kutoka kwa serikali ya Uingereza imetahadharisha dhidi ya safari za kuelekea Sinai ya Kaskazini kwa sababu ya utovu wa usalama katika eneo hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi