Mbunge Zungu aeleza sababu ya kumwita Waziri Lugola kukamata Mateja jimboni kwake


Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu ameeleza sababu ya kumwita Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kufanya operesheni ya kuwasaka na kuwakamata mateja mbalimbali ambao wanatumia dawa za kulenya na kufanya uhalifu katika bonde la Jangwani, Ilala, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza hii leo amesema wahalifu hao hawatoki pekee katika Jimbo lake, bali wengi wao
wanatoka maeneo mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam.

“Wenyeji wa eneo hili ni wachache, wengi wanatoka mitaa mbalimbali ya hapa Dar es Salaam ikiwemo Temeke na kwingineko, hivyo mheshimiwa Waziri tunajua utendaji wako, tunakuomba hii kero inatuumiza sana, wananchi wanakosa amani kutokana na uwepo mkubwa wa wahalifu
hawa,’ alisema Zungu.

Waziri Lugola alisema Dkt John Magufuli anawataka wananchi wake waishi kwa amani na utulifu, yeye Waziri hatakubali kuona matukio hayo ya baibu yakishika kasi mitaani. Aliwataka Makamanda wa Polisi nchini kuwasaka wahalifu muda wowote si mpaka yeye atoe agizo au atembelee
Mpya zaidi Nzee zaidi