Maabara ya anga la juu China yazidi kupata mafanikio makubwa


Shirika la Anga ya Juu la China limesema maabara ya anga ya juu ya China Tiangong-2 imeingia tena kwenye udhibiti wa anga hewa ya dunia jana majira ya saa tatu usiku kwa saa za Beijing.

Shirika hilo limeeleza kuwa mabaki machache ya chombo hicho cha anga ya juu yalidondoka kwenye sehemu salama iliyokadiriwa ya bahari ya kusini ya Pasifiki.

Msanifu mkuu wa programu ya anga ya juu ya China, Zhou Jianping amesema kuingia kwa udhibiti kwenye anga hewa ya dunia kwa Chombo cha Tiangong-2, kunaonesha kukamilika kwa mafanikio kwa kazi zote kwenye maabara ya anga ya juu za programu ya anga ya juu ya China. Ameongeza kuwa juhudi zinaendelea kufanywa ili kuharakisha maandilizi ya ujenzi wa kituo cha anga ya juu cha China.
Mpya zaidi Nzee zaidi