RC Mwandri na Diamond Platnumz waongoza vijana kupatiwa elimu kuhusu UKIMWI


Mapema hii leo Wasanii wanaoshiriki Tamasha la Wasafi Festival 2019 wakiongozwa na Diamond Platnumz waliungana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwandri kutembelea Chuo cha Musoma Utalii College kilichopo Mkoani humo.

Elimu kuhusu UKIMWI imetolewa, kampuni mbalimbali yametoa elimu na msaada pia. Lengo likiwa kurudisha hisani kwa jamii, kutoa elimu ya VVU na UKIMWI pamoja na kuhamasisha upimaji wa virusi vya UKIMWI haswa kwa Vijana.

Mkuu wa Tabora, Agrey Mwandri  amesema kuwa kupitia Tamasha la Wasafi Festival 2019 vijana wengi watapata elimu na kujua namna gani wanaweza kujikinga na VVU kwa mkoa huo.


Mpya zaidi Nzee zaidi