Alex Iwob kuihama Arsenal iwapo hili litafanikiwa


Mchezaji wa Arsenal, Alex Iwobi amesema ataihama klabu hiyo endapo itafanikiwa kumsaini Wilfe5 Zaha kutoka Crystal Palace. Arsenal imeonesha nia dhabiti ya kutaka kusajili Zaha japo bado hawajafikia dau la usajili ambalo Palace wanalihitaji.

Iwobi baada ya kumaliza michuano ya AFCON 2019, alivyoulizwa kuhusu hatma yake ndani ya Arsenal akasema kwa muda mrefu amekuwa anaamini anastahili kusubiri nafasi yake ya kucheza kwa sababu hakuwa na uhakika wa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Lakini sasa hivi anaamini huu ndio wakati sasa yeye kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza lakini hizi taarifa za klabu yake kutaka kumsajili Zaha kama zitakamilika inamaana yeye kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza itazidi kupungua na maamuzi sahihi ni kuondoka ili akatafute nafasi ya kucheza sehemu nyingine.