Loading...

Jul 21, 2019

Waziri Mkuu alipongeza Kanisa la Tanzania Assemblies of God


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelipongeza Kanisa la Tanzania Assemblies of God kwa kuthamini na kutambua kazi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.

“Baba Askofu Mtokambali umenifurahisha kwa takwimu ulizozitaja hapa za miradi mikubwa ambayo inatekelezwa na Serikali hii. Kuna wengine hawapendi kusikia mambo kama haya, hongera sana,” amesema.

Ametoa pongezi hizo leo mchana wakati akizungumza na maelfu ya waumini wa kanisa hilo katika maadhimisho ya miaka 80 ya TAG hapa nchini yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli, amesema ameguswa na jinsi kanisa hilo linavyomtambua Mheshimiwa Rais na wasaidizi wake na kuthamini juhudi za Serikali.

“Serikali hii imedhamiria kuwatumikia Watanzania wote bila kujali dini zenu, rangi wala itikadi za kisiasa. Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kumtegemea Mungu pasipo shaka yoyote.”

Pia amewapongeza viongozi wa kanisa hilo kwa mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chote cha miaka 80.

“Pia nikupongeze Baba Askofu kwa kuchangia mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari hapa Arusha. Natambua kwamba ulishachangia mifuko mingine 500, asante sana.”KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger