Aliyekuwa Naibu Kamanda wa Jeshi la Uganda, Luteni Jenerali Peter Elwelu, amekamatwa kufuatia operesheni iliyodumu kwa wiki moja katika eneo la Teso, mashariki mwa Uganda.
Baada ya kustaafu jeshi miaka miwili iliyopita, Elwelu alianza kuikosoa Serikali, hasa masuala ya rushwa, ukosoaji wake ukimfanya mkuu wa majeshi, Muhoozi Kainerugaba kuagiza atafutwe.
Elwelu, ni miongoni mwa watu waliowekewa vikwazo na Marekani kwa kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu, kufuatia mauaji yaliyotokea katika Ufalme wa Obusinga Bwa Rwenzururu.
