RC Sirro aagiza uchunguzi ajali ya moto Soko la Mwandiga



Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro ameagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto uliounguza vibanda 15 katika Soko la Mwandiga lililopo katika Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.

Jumla ya vibanda 10 vilivyokuwa vikitoa huduma ya tiba Asili, duka moja la vitenge, duka la dawa baridi za binadamu, stoo moja ya mazao ya chakula pamoja na maduka mawili ya nafaka, vimeteketea kutokana na moto huo.

Mara baada ya kukagua eneo hilo Balozi Sirro ametoa wito kwa wamiliki wa maduka kuchukua tahadhari kwa kutochoma vitu kama vile mishumaa au udi na kuviacha vikiwaka kwa muda mrefu ndani ya maduka.

Aidha, ametoa pole kwa waliopata hasara na kuahidi kuchukua hatua baada ya kukamilika kwa uchunguzi utakaobaini chanzo cha tukio hilo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi