Apewa elfu 20 baada ya kusalimisha silaha haramu


Mkazi wa Kijiji cha Mafisa, Kata ya Mvungwe, Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Juma Hamisi Msilagi, mwenye umri wa miaka 69, amesalimisha kwa hiari silaha moja aina ya gobore inayomilikiwa kinyume cha sheria, kufuatia wito wa kusalimisha silaha haramu uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Patrobas Katambi.

Katika kuhamasisha wengine kuendelea kusalimisha silaha hizo kwa hiari, mwananchi huyo amezawadiwa kiasi cha shilingi 20,000 na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kilindi, ASP Mtera.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Jeshi la Polisi kuhamasisha wananchi kuitikia wito wa msamaha kwa kusalimisha silaha wanazomiliki kinyume cha sheria kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika jamii.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi